Monday, December 13, 2010

Bado waandika script washindwa kukutana

Chama cha waandika story na script za Filamu nchini TASA wameshindwa kufanya kikao chao ambacho kilikuwa kifanyike terehe 2/12/2010. na kuahirishwa hakijapata kufanyika na wala haijapangwa ni lini kitafanyika.

Director Ramadhani Kigalu alalamikia waandishi

Director wa Filamu wa siku nyingi hapa mjini bwana Ramadhani Kigalu amewalalamikia waandishi wa habari wanaotafuta mabaya tu na kuyaandika na kusahau kuandika mazuri wanayo yafanya wasanii wa filamu hapa nchini. Akizungumza katika Jukwaa la sanaa linalofanyika kila siku ya jumatatu katika ukumbi wa  baraza la sanaa BASATA  bwna Rama alisema "kuna baadhi ya waandishi kazi yao kutafuta mabaya tu katika kazi zetu tukifanya mazuri hawaandiki hii inafanya kutudidimiza sana sisi wasanii kwenye Tasnia yetu"

chiki apata jiko

Msanii wa filamu nchini bwana chiki aliuaga ukapela baada ya kupata jiko siku ya jumamosi ya tarehe 11/12/2010.. Harusi hiyo iliyofana ilifanyika katika ukumbi wa msasani beach club iliudhuliwa na wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu nchini. akiwemo mzee kipara. Blog hii ya Tollywood today inawatakia maisha marefu na yenye furaha Chiki na Mkewe



chiki na mkewe wakikamata maaku;i


Kanumba akimpongeza chiki

Friday, December 10, 2010

kanumba na UNCLE JJ Ray na Family Disaster

Manguli wa Filamu nchini Tanzania Kanumba na Ray wanafunga mwaka kwa kutupa kazi zao sokoni. Huku kanumba akichomoka na UNCLE JJ, Ray yeye amedondosha Familiy Disaster. Kama haitoshi wote kwa pamoja wanaandaa Filamu nyingine iitwao OFFSIDE watakayo washirikisa Irene Uwoya na Unt Ezekiel




posta ya UNCLE JJ kamainavyonekana



Maswahiba Kanumba na Ray wakibonyea misosi



Kanumba na Ray Ndani ya OFFSIDE

karibuni wote

napenda kuwakaribisha  wote katika blog hii ya Tollywood ambayo inamilikiwa na mimi Prosper William Lyimo ambapo mtakuwa mkijipatia habari mbalimbali, wasanii wapya,msanii wa siku movie mpya na mambo mbalimbali kutoka Tollywood. au bongo movie.



Karibuni sana.