tollywoodtoday
Monday, December 13, 2010
Bado waandika script washindwa kukutana
Chama cha waandika story na script za Filamu nchini TASA wameshindwa kufanya kikao chao ambacho kilikuwa kifanyike terehe 2/12/2010. na kuahirishwa hakijapata kufanyika na wala haijapangwa ni lini kitafanyika.
Director Ramadhani Kigalu alalamikia waandishi
Director wa Filamu wa siku nyingi hapa mjini bwana Ramadhani Kigalu amewalalamikia waandishi wa habari wanaotafuta mabaya tu na kuyaandika na kusahau kuandika mazuri wanayo yafanya wasanii wa filamu hapa nchini. Akizungumza katika Jukwaa la sanaa linalofanyika kila siku ya jumatatu katika ukumbi wa baraza la sanaa BASATA bwna Rama alisema "kuna baadhi ya waandishi kazi yao kutafuta mabaya tu katika kazi zetu tukifanya mazuri hawaandiki hii inafanya kutudidimiza sana sisi wasanii kwenye Tasnia yetu"
chiki apata jiko
Msanii wa filamu nchini bwana chiki aliuaga ukapela baada ya kupata jiko siku ya jumamosi ya tarehe 11/12/2010.. Harusi hiyo iliyofana ilifanyika katika ukumbi wa msasani beach club iliudhuliwa na wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu nchini. akiwemo mzee kipara. Blog hii ya Tollywood today inawatakia maisha marefu na yenye furaha Chiki na Mkewe

chiki na mkewe wakikamata maaku;i

Kanumba akimpongeza chiki

chiki na mkewe wakikamata maaku;i

Kanumba akimpongeza chiki
Friday, December 10, 2010
kanumba na UNCLE JJ Ray na Family Disaster
Manguli wa Filamu nchini Tanzania Kanumba na Ray wanafunga mwaka kwa kutupa kazi zao sokoni. Huku kanumba akichomoka na UNCLE JJ, Ray yeye amedondosha Familiy Disaster. Kama haitoshi wote kwa pamoja wanaandaa Filamu nyingine iitwao OFFSIDE watakayo washirikisa Irene Uwoya na Unt Ezekiel

posta ya UNCLE JJ kamainavyonekana

Maswahiba Kanumba na Ray wakibonyea misosi

Kanumba na Ray Ndani ya OFFSIDE

posta ya UNCLE JJ kamainavyonekana

Maswahiba Kanumba na Ray wakibonyea misosi

Kanumba na Ray Ndani ya OFFSIDE
karibuni wote
napenda kuwakaribisha wote katika blog hii ya Tollywood ambayo inamilikiwa na mimi Prosper William Lyimo ambapo mtakuwa mkijipatia habari mbalimbali, wasanii wapya,msanii wa siku movie mpya na mambo mbalimbali kutoka Tollywood. au bongo movie.
Karibuni sana.
Karibuni sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)